Dampo Terms

SHERIA NA MASHARTI YA MATUMIZI – DAMPO APP

1. UTANGULIZI
Karibu kwenye Dampo! Hizi ni Sheria na Masharti ya matumizi ya programu yetu ya Dampo (“App”). Kwa kutumia App hii, unakubaliana na masharti haya. Tafadhali yasome kwa uangalifu kabla ya kutumia huduma zetu.


2. MATUMIZI YA APP
a) Dampo ni jukwaa linalosaidia watumiaji kuripoti taka, kupanga ratiba za ukusanyaji taka, kushiriki kwenye kampeni za usafi, na kupata motisha kupitia zawadi.
b) Watumiaji wanawajibika kutoa taarifa sahihi wanaposajili akaunti zao.
c) Ni marufuku kutumia App kwa shughuli zisizo halali au zinazohatarisha mazingira.

d) Watumiaji wanaweza kuona ratiba za ukusanyaji wa taka, kuangalia ramani za dampo zilizo karibu, kuripoti taka, kupanga na kuomba taka kuja kuchukuliwa kwa kulipia gharama kidogo.


3. ULINZI WA FARAGHA NA DATA
a) Dampo inaheshimu faragha ya watumiaji na inazingatia sheria za ulinzi wa data.
b) Maelezo ya watumiaji yatatumika tu kwa madhumuni ya kuboresha huduma.
c) Taarifa za mtumiaji hazitagawanywa kwa watu wa tatu bila idhini ya mtumiaji, isipokuwa kwa mujibu wa sheria.


4. MAJUKUMU YA MTUMIAJI
a) Watumiaji wanapaswa kutumia App kwa uaminifu na uadilifu.
b) Ni jukumu la mtumiaji kuhakikisha taarifa anazotoa zinahusiana na mazingira halisi.
c) Watumiaji wanapaswa kushiriki katika shughuli za usafi kwa mujibu wa sheria na kanuni za mazingira.


5. KUKUSANYA NA KUSHUGHULIKIA TAKA
a) Dampo inashirikiana na mamlaka husika katika ukusanyaji wa taka.
b) Watumiaji wanapaswa kuheshimu ratiba za ukusanyaji taka na kuziweka taka kwenye maeneo yaliyotengwa.
c) Dampo haina wajibu wa kukusanya taka moja kwa moja bali inaratibu na kushirikiana na mamlaka zinazohusika.
d) Dampo inaweza kuwa na magari yake ya ukusanyaji wa taka na kufanya shughuli za ukusanyaji taka moja kwa moja.
e) Dampo inashirikiana na madereva wa manispaa au halmashauri husika kwa kutumia mfumo huu wa App.
f) Dampo inaweza kusajili madereva binafsi wenye magari yao kwa ajili ya kubeba taka.
g) Mtumiaji anaweza kuomba huduma ya premium ya kwenda kuchukuliwa taka, ambapo atatakiwa kulipa gharama husika kupitia App.


6. HAKI NA WAJIBU WA DAMPO
a) Dampo ina haki ya kufanya mabadiliko kwenye App bila kutoa taarifa ya awali.
b) Dampo haitawajibika kwa hasara yoyote inayotokana na matumizi mabaya ya App.
c) Dampo inaweza kusimamisha au kufuta akaunti za watumiaji wanaovunja masharti haya.


7. USHIRIKIANO NA WADHAMINI
a) Dampo inaweza kushirikiana na mashirika mbalimbali kwa lengo la kuboresha huduma.
b) Wadhamini na washirika hawana mamlaka ya kubadilisha masharti haya bila idhini ya Dampo.


8. MABADILIKO YA SHERIA NA MASHARTI
a) Dampo inaweza kusasisha masharti haya mara kwa mara.
b) Watumiaji watajulishwa kuhusu mabadiliko yoyote kupitia App au barua pepe zao.
c) Kuendelea kutumia App baada ya mabadiliko inamaanisha umekubaliana na masharti mapya.


9. MAWASILIANO
Kwa maswali au maoni kuhusu Sheria na Masharti haya, tafadhali wasiliana nasi kupitia:
📩 Barua pepe: info@dampoapp.com
📞 Simu: +255 763 155 863

Kwa kutumia Dampo, unakubaliana na Sheria na Masharti haya. Asante kwa kushiriki nasi katika kutunza mazingira!

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top